Asante Kwasi azipasua kichwa Simba na Lipuli - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday 20 December 2017

Asante Kwasi azipasua kichwa Simba na Lipuli




NA ISSA RAMADHANI.
KLABU ya soka ya Lipuli FC hapa nchini imesema mlinzi wao Asante Kwasi (PICHANI) ,bado ni mchezaji wao halalia katia kikosi hicho na alitakiwa kuripoti kambini tangu Disemba 16 mwaka huu lakini hajafanya katika hivyo hadi sasa.

Aidha Lipuli kupitia kwa msemaji wake Clement Sanga amesema taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa mchezaji huyo raia wa Ghana amejiunga na klabu ya Simba sio za kweli kwani bado anamkatabna na timu hiyo.
“Asante Kwasi tulimpa ruhusa ya kuhudhuria msiba wa baba yake nyumbani kwao Gahan na alitakiwa kurudi Disemba 16 na tulifuata taratibu zote ikiwemo kumtumia pesa ya tiketi ya ndege pamoja na mshahara wa mwezi uliopita lakini hadi sasa hajafika hivyo tunashindwa kuelewa”, amesema Sanga.

Siku za hivi karibuni haswa wakati huu wa dirisha dogo la usajili kumekuwepo na taarifa mbalimbali, kuwa mlinzi huyo ambaye amefunga mabao matano hadi sasa kwenye ligi kuu, amesajiliwa na klabu ya Simba japo vinara wa ligi hiyo hawajatoa taarifa juu ya usajili wao.

Hata hivyo tayari Lipuli imeshaweka hadharani majina ya wachezaji walioachwa na waliosajiliwa kwenye dirisha dogo. Kwa walioachwa ni Waziri Ramadhani, Mussa Ngunda, Machaku Salum, Melvin Alistoto, Dotto Kayombo  na Ahmeid Manzi.
Kwa waliosajiliwa ni Jamal Mnyate kwa mkopo kutoka Simba, Adam Salamba kutoka Stand United, Alex Ntiri kutoka Mbao FC ambaye ni raia wa Ghana, Miraji Mwilenga na Awadi Mauya kutoka Mufindi United pamoja na Steven Mganga kutoka Pamba FC


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot