`Serikali irejee mkataba mauzo ya mbaazi India’ - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday 1 November 2017

`Serikali irejee mkataba mauzo ya mbaazi India’

NA MOHAMEDI NG`OULA .
                                    
CHAMA cha  Siasa cha ACT  Wazalendo  kimemshauri Waziri wa Viwanda  na Biashara,  Charles Mwijage kusimamia bei ya zao la mbaazi kutokana na umuhimu wa zao hilo katika kukuza kipato cha mwananchi na taifa.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Charles Mwijage(kulia) akipata maelezo kwa mwendesha mitambo wa kampuni ya TBL, Mecky Mlay alipotembelea.

Ushauri huo jijini Dar es salaam na Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi  wa chama hicho Ado Shaibu,  wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari  juu  ya utafiti ulifanywa na chama hicho kuhusu hali ya soko la mbaazi  hapa nchini.

Akifafannua, alidai kuwa serikali inasuasua kutumia mkataba  kati yake na India wa kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuuza mbaazi nchini humo kitendo ambacho kinasababisha wakulima kukosa uhakika wa kilimo kutokana na kusuasua kwa bei.

Wakulima wa kilimo cha pamba pichani. 

Kwa mujibu wa katibu huyo, uzalishaji mkubwa wa mbaazi nchini umechochewa na India kabla na wakati wa ujio wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi hapa nchini  ambapo wakulima na wafanyabiashara walihakikishiwa soko, ingawa  suala hilo halikutiliwa mkazo na mbaazi nyingi za wakulima kuozea shambani.

 “Tulielezwa kwamba Tanzania haistahili kuzuiwa mbaazi zake kwa sababu zuio husika haligusi nchi zenye  mahusiano mahususi na kuuza mazao India. Sisi tuna makubaliano ya kupeleka mazao India wa mwaka 2000… ni jambo la kushangaza kuwa serikali imeshindwa kulifuatilia tangu lilipo jitokeza mwezi wa nane mwaka huu,”alisema Shaibu.

Katibu huyo, alisema alisisitiza umuhimu wa serikali  kutafuta masoko mapya ya zao la mbaazi kwenye nchi  tofauti na India kama vile Afrika Kuusini, Canada, Uingereza na Marekani na kutumia mkataba wa India ili kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuuzia mbaazi nchini humo.

“Serikali ifanye mazungumzo na serikali ya India  ili kuwanusuru wakulima, tunatambua Tanzania na India ni marafiki tangu uhuru wa Taifa letu, ni vyema  tuyatumie  mahusiano haya kuhakikisaha tunalinda soko la wakulima wetu sambamba na kutafuta masoko kwinginepo kwa kutumia mkataba huu ili kuziaminisha nchi hizo uhakika wetu wa uzalishaji, ”.alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Katibu huyo wa ACT alishauri kufunguliwa kwa viwanda vya usindikaji wa bidhaa zinazotokana na mbazi kama biskuti na keki badala ya kufikiria kuuza nje pekee jamboa ambalo haliakisi kuongeza ajira na  sera ya Taifa la Viwanda.


Hivi karibuni zao la mbaazi limekuwa likilalamikiwa kushuka  kutoka Shilingi  2, 500 kwa kilo  msimu wa mwaka 2016 hadi shilingi 2,000 kwa kilo kwa mwaka huu kwenye mikoa mbalimbali nchini jambo ambalo limewaathiri wa wakulima wengi kutokana na kulima mbaazi kwa wingi huku soko likisuasua na kusababisaha hasara kubwa. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot