Urusi imefungiwa kushiriki michuano ya Olimpiki mwakani. - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, 6 December 2017

Urusi imefungiwa kushiriki michuano ya Olimpiki mwakani.

SWITZERLAND, Lausanne

KAMATI  ya kimataifa ya Olimpiki, imeifungia nchi ya urusi kushiriki michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi itayofanyika katika jiji la Pyeongchang nchini Korea kusini mwakani 2018.

Hata hivyo Rais wa IOC Thomas Bach na bodi yake walitangaza adhabu hiyo jana jioni baada ya kukutana katika mji wa Lausanne nchini Switzerland, maamuzi hayo yamefikiwa baada ya uchunguzi wa miezi kumi na saba.

Image result for Rais wa IOC Thomas Bach
Rais wa IOC Thomas Bach
Serikali ya Urusi ilihusika katika udanganyifu wa kuanda michuano ya olimpiki iliyofanyika nchini humo mwaka 2014 pamoja na udanganyifu kuhusu matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.

Aidha Uchunguzi huo ulikuwa ukiongozwa na Rais wa zamani wa IOC Samuel Schmid, Licha adhabu hiyo wanariadha wa Urusi wanaweza shiriki michuano ya majira ya baridi kama wanariadha huru ambao watakuwa wakiwakilisha nchi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot