Timbulo Ampa Tano Alikiba Amkosoa Diamond - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, 4 December 2017

Timbulo Ampa Tano Alikiba Amkosoa Diamond

MSANII  wa muziki wa Bongo Flava nchini, Timbulo amesema wasanii wa Tanzania  wajifunze kutoa kazi zao kwa lengo la kujitangaza nje ya nchi kuliko kutengemea wasanii wa nje pekee,ambao muda mwingine hawana mchango wowote.



Image result for TIMBULO Aidha Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Vibaya’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa mfano mzuri kolabo ya Diamond na Davido kwani kolabo hiyo ilimtangaza zaidi Davido hapa nchini kuliko Diamond nchini Nigeria.

“Kumshirikisha msanii wa nje ni kumleta hapa, tumemjua Davido baada ya kushirikishwa na Diamond baada hapo Davido alikuwa kama Mtanzania vile, anavyopingwa utasema anatokea Manzese vile lakini Davido hakumsaidia kule. Chukua mziki upeleke kule, Darassa ame-trend mpaka Afrimma hakumshirikisha msanii yeyote wa nje” amesema Timbulo.

Timbulo aliendelea kwa kusema Alikiba ameweza kushinda tuzo bila kolabo na msanii wa nje  na kueleza hivyo ndivyo inatakiwa.

“Mfano Turudi hapa hapa, Alikiba amefanya kazi nyingi na amefikia hatua amechukua tuzo za MTV si kwa kolabo ni kazi za nyumbani, kwa hiyo tunaweza kufanya siyo lazima kolabo nje watu wasikariri” amesisitiza. 


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot