NA MWANDISHI WETU,
KATIKA kubana na kupunguza gharama za uendeshaji na
kurahisisha usambazaji wa bidhaa yake, kampuni ya Dangote imeingia mkataba na
Jumia Nigeria ili kuanza kuuza saruji kupitia mtandao huo.
Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo ambayo imewekeza pia nchini inasema Wanigeria au kampuni zitakazotaka kununua kuanzia tani 15 au mifuko 300 ya kilo 50 zinaweza kutoa ‘oda’ zao kupitia mtandao huo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo baada ya kutoa ‘oda’ mzigo utawasilishwa kwa punguzo la bei tofauti na iliyopo madukani.
Mkurugenzi wa fedha wa Dangote, Chux Mogbolu alisema ushirikiano huo utaifanya saruji yao iwe inapatikana popote nchini humo hata sehemu ambazo hazina mawakala.
Kwa kuanzia, alisema huduma hiyo itakuwa inapatikana katika miji ya Lagos, Port- Harcourt na Abuja.
“Dangote imeichagua Jumia kutokana na uadilifu wake kufanikisha bishara mtandaoni kwa miaka mingi. Ushirikiano huu utaondoa utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu kwenye saruji yetu,” alisema.
Kadri uhitaji utakavyoongezeka, alisema huduma hiyo itaenea kwenye mikoa mingine ili kuwapa fursa wananchi kuagiza na kulipia mtandaoni wakisubiri kuwasili kwa mizigo yao.
Mogbolu alieleza kuwa kwa kuanza wateja wanaotaka kuanzia tani 15, 30 au 45 watahudumiwa huku kukiwa na uwezo wa kuwahudumia wanaotaka mzigo mkubwa zaidi.
Ofisa mtendaji mkuu wa Jumia, Juliet Anammah alisema ushirikiano huo ni mwendelezo wa kuaminika kwa mtandao huo katika kufanikisha biashara bila chembe ya wasiwasi kati ya muuzaji na mnunuzi.

Baada ya mazungumzo ya kina na Serikali, mmiliki wa kiwanda hicho, Aliko Dangote alikubali kuwekeza nchini na kilizinduliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Oktoba 2015.
Kutokana na ukubwa wa uwekezaji huo, kiwanda hicho kinaelezwa kuwa ndicho kikubwa zaidi Afrika Mashariki. Licha ya kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa hiyo, kiwanda hicho kimechangia upatikanaji wa maelfu ya ajira kuanzia kwenye shughuli za uzalishaji na usambazaji.
No comments:
Post a Comment