Tanesco watoa taarifa kukatika kwa umeme Dar, Pwani - ISSRADHANS

Umoja na uzalendo

Umoja na uzalendo

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, 29 November 2017

Tanesco watoa taarifa kukatika kwa umeme Dar, Pwani

NA MWANDISHI WETU,


SHIRIKA  la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa taarifa kwa wateja katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuwa baadhi ya maeneo hayana umeme kutokana na hitilafu iliyojitokeza.
Taarifa ya Tanesco imesema baadhi ya maeneo ya mikoa hiyo hayana umeme kuanzia saa 3:20 asubuhi ya leo Jumatano Novemba 29,2017 kutokana na mashine namba tatu ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia kituo cha Ubungo II kupata hitilafu.

“Mafundi wa shirika wanaendelea na jitihada za kutatua hitilafu hiyo kwa haraka ili kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida,” imesema taarifa ya Tanesco.

Shirika hilo limesema litaendelea kutoa taarifa za maendeleo ya kazi hiyo.

Pia, Tanesco imetoa tahadhari kwa wananchi kutosogelea, kushika wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot