KENYA,NAIROBI
Mamlaka ya Usalama wa Uchukuzi nchini Kenya NTSA
imependekeza adhabu mpya miongoni mwa madereva walevi.
Madereva walevi sasa watalazimika kufanya kazi
katika vyumba vya kuhifadhia maiti ili kupunguza idadi kuu ya ajali za
barabarani.
”Hatuwezi kuwa na madereva wengi walevi wanaofanya
ajali na wanapofikishwa mahakamani wanapewa adhabu hafifu.Tutakapokamilisha
kutengeza sera hiyo mpya tutahakikisha kuwa inakuwa sheria”, alisema mkurugenzi
wa mamlaka hiyo Francis Meja.
Na Wakenya wengi katika mitandao ya kijamii waliunga mkono mpango huo na kusema kuwa utawafanya madereva kuwa makini.

No comments:
Post a Comment