MSANII wa muziki bongo fleva nchini ambaye anafanya vyema na wimbo wake 'Seduce me' Jina
la Alikiba ameamua kuachia video ya wimbo wake wa zamani ambao ulivuja kama
zawadi kwa mashabiki wake katika siku yake ya kuzaliwa.
Alikiba jana alikuwa anasherehekea
kumbukumbu ya mwaka wa kuzaliwa aliamua kuachia video ya wimbo wa 'Maumivu Per Day' kama njia ya
kusherekea siku hiyo na mashabiki zake.
"Nashukuru sana watu ambao
wamenitakia kheri katika siku yangu ya kuzaliwa, nimejaliwa, kupendelewa na
kupendwa pia nashukuru sana kwa jambo hilo, nawapenda wote na nitafanya kazi kwa
nguvu zote kuwafanya mjivunie uwepo wangu.
"Maumivu Per Day ni kati ya
nyimbo zangu za zamani zinazopendwa nimeamua kuitoa japo siyo rasmi ili
kusherehekea kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa na mashabiki zangu"
alisema Alikiba
No comments:
Post a Comment