NA ODRIAN NICOLAUS
SERIKALI imeombwa kupunguza bei za dawa za kutibia
mifugo na kusimamia bei elekezeki kipindi dawa zinapofika kwa mawakala hii ni
kutokana n kupanda kwa ghrama kila siku na kusababisha huduma kuwa ngumu.
Akizungumza na gazeti hili, Dk. Wa mifugo kutoka
mkoani Kilimanjaro, Nicolaus Gerald, alisema kuwa Serikali inatakiwa kutazama
upya swla la kupanda kwa gharama za dawa za mifugo kwani ni moja ya sekta
ambayo wtu wengi wameamua kujikita katika kujiajiri.
Aidha, Dk.
Gerald alisema wataalamu wa Vijini kwa sasa wanatakiwa kukabilaiana kutokana na
mabadiliko ya tabia ya nchi na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia na wajenge
utaratibu wa kutembeleana kufika katika maeneo husika tofauti na hapo nyuma
walikuwa wanakaa ofisini au wakiitwa kipindi matatizo yanapotokea.
Dk. Gerald, alitoa ushauri huku aikiomba Serikali iwatazame
kwa karibu wataalamu waliojitolea na kutoa huduma Vijijini kwa kuwasaidia
usafiri waweze kutoa huduma kwa urahisi ikiwamo kutembelea nyumba kwa nyumba wakitoa
elimu ya namna bora ya ufugaji.
![]() |
| Dk. Gerald |
Mkazi mmoja ambaye anajihusisha na ufugaji wa kuku,
Remi Mtei, alisema kuwa anawashukuru wataalamu wa mifugo kwa kujitolea
kufundisha elimu hiyo kwani ni faida kwao katika kuendesha maisha yao.
“Kupitia wataalamu binafsi nimefurahi sana kunipatia
mifugo yangu chanjo na njia za kisasa za ufugaji, hivyo kil baada ya miezi
mitatu wanapokuja wanaturahisishia kutambua vizuri ufugaji pamoja na changamoto
zinazotukabili ila sitosita kuwapongeza”alisema Mtei
.Upo umuhimu wa Serikali kutizama matatizo ya
Wajasiriamali na wataalamu wanaoamua kujiajiri kwa karibu ili waweze kuleta
Taiafa lenye maendeleo na kuamsha ari kwa Vijana wengine kuchangamkia fursa.

No comments:
Post a Comment