
MADRID,HISPAIN
MCHEZAJI
wa zamani wa Klabu ya soka ya Tottenham, Luka Modric ameripotiwa huenda akarudi
kwenye timu yake ya zamani ya Tottenham Mwishoni mwa msimu huu.
Modric mwenye
umri wa miaka 32, ni miongoni mwa wachezaji
wengi waliovutia katika historia ya
Tottenham baada ya kufanya vyema kunako timu yake ya Taifa ya Kikroeshia licha
ya kuwa na wakati mbaya Madrid.
Mchezaji huyo, alifanikiwa kushinda ligi ya Mabingwa
mara tatu huku akionekana kama moja ya kivutio bora duniani.
Hivi sasa klabu yake ya Madrid haijui hatma ya
mchezaji huyo pamoja na kukosa nafasi ya
kucheza kwenye kikosi cha kwanza .
Nyota huyo anatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu
huu licha ya kufukuziwa na Vilabu kama vile Inter Milan na Manchester United
lakini uwezekano mkubwa upo Tottenham kwa sababu nyingi.
No comments:
Post a Comment