NA
RASHID HASSAN
MENEJA
wa zamani wa Uwanja wa CCM Kirumba na mzazi wa mshambuliaji wa soka wa timu ya
Maji Maji ya Songea, Jerrson Tegete, Mzee John Tegete, amewapongeza chuo cha
kukuza vipaji (academia) ya Alliance ya mwanza kwa kupanda ligi kuu ya
Vodacom.
Tegete, alisema ni pongezi na mabadiliko makubwa kwa
soka la Tanzania, kwani Alliance walionesha ukomavu mkubwa wa kisoka na kuwa
Akademia pekee iliyowahi kupanda ligi kuu bara hapa nchini kwa miaka ya hivi
karibuni.
wachezaji wa Timu ya Alliance |
Akizungumza na
mwandishi leo , Mzee Tegete, alisema Alliance imefanikisha ndoto za mkurugenzi
wao ambaye ni Meya wa Jiji la Mwanza ,
James Bwire, ambapo anaamini watafanikiwa kufanya vizuri kwani wanavipaji vingi
ukizingatia wengine wapo chuoni.
Alisema, anaamini Mkurugenzi wa Alliance, atafuata
matakwa ya wachezaji wa ligi kuu ya Vodacom, akiwapatia wachezaji wake mikataba
pamoja na kuingizwa katika ajira rasmi itakayowawezesha kumudu hali ya kiuchumi
iliyopo na familia zao.
“Vijana wamepiga hatua kubwa sana, pamoja na
changamoto walionesha nia ya dhati ya kutaka kuingia ligi kuu, nawaomba
waendele na umoja wao na mshikamano kama walivyofanya ligi ya FDL, na hakika
watafanikiwa na wataitangaza vyema mkoa wa Mwanza na na Taifa kwa ujumla”,
alisema Tegete
Mbali na hayo, alimpataka Mkurugenzi wa Alliance,
ktafuta wazoefu watakaoongeza morali ya kiushindani licha ya kuwepo na vipaji
lukuki lakini haitawasaidia kuhimili mikiki mikiki ya ligi kuu ya Vodacom.
Pia aliitaka TFF, kugeukia Alliance wakati wa uteuzi
wa timu ya Taifa na ile ya Vijana kwani anaamini chuo hicho cha vipaji kina
vijana wengi wenye uwezo zaidi ya wale wanaoitwa timu ya Taifa na waliokatika
ligi kuu ya Tanzania bara.
Alliance FC, ilifanikiwa kupanda ligi kuu bara ikiwa
na alama 28 kwenye kundi ‘C’ nyuma ya Biashara ya mara ambao walikuwa kinara wa
kundi hilo.